Viongozi wa UDA Kitui watetea ushirikiano na Serikali ya Kenya Kwanza, wasisitiza maendeleo

KITUI: Viongozi wanaounga mkono Serikali ya Kenya Kwanza wameendelea kutetea ushirikiano na Serikali ya Kitaifa wakisema umechangia kuharakisha maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Kaunti ya Kitui kupitia miradi inayotekelezwa chini ya uongozi wa Rais William Ruto.

Wakiongozwa na Mbunge wa Kitui Kusini Dkt. Rachael Kaki Nyamai na afisa wa UDA Moses Mbanda, pamoja na viongozi wengine, walisema wananchi wanapaswa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Kitaifa ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kunufaisha jamii.

Viongozi hao walitoa kauli hizo katika Soko la Twimyua, Wadi ya Kyuso, Kaunti Ndogo ya Mwingi Kaskazini, wakati wa hafla ya kuwawezesha kiuchumi vikundi vya wanawake.

Walisema Serikali ya Kenya Kwanza imeonyesha dhamira ya kupeleka maendeleo katika sehemu zote za nchi bila ubaguzi, wakitaja ujenzi wa miundombinu, masoko ya kisasa, taasisi za mafunzo na miradi mingine ya maendeleo kama ushahidi wa mafanikio ya ushirikiano kati ya viongozi na Serikali ya Kitaifa.

Aidha, viongozi hao waliwahimiza wananchi kuendelea kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya Rais William Ruto, wakisema ushirikiano ndio njia bora ya kuhakikisha miradi iliyoanzishwa inakamilika na fursa zaidi za maendeleo zinapatikana kwa wananchi.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *